Sign Up

Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Have an account? Sign In

Have an account? Sign In Now

Sign In

Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection

Sign Up Here

Forgot Password?

Don't have account, Sign Up Here

Forgot Password

Lost your password? Please enter your email address. You will receive a link and will create a new password via email.

Have an account? Sign In Now

Please type your username.

Please type your E-Mail.

Please choose an appropriate title for the question so it can be answered easily.

Please briefly explain why you feel this answer should be reported.

Sign InSign Up

1Sky

1Sky

1Sky Navigation

  • Blog
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App

Mobile menu

Close
Ask a Question
  • Home
  • Maswali
  • Points
  • Miongozo
  • Wasiliana Nasi
  • Advanced Search
  • App
Home» Questions»Q 30126
In Process
Adv
Anonymous
Asked: February 27, 20192019-02-27T07:33:52+03:00 2019-02-27T07:33:52+03:00In: Afya

Kwa nini naumwa tumbo nikiwa period?

Kwa nini naumwa tumbo nikiwa period?
  • 1
  • 1,091
  • 0
  • Share
    • Share on WhatsApp
    • Share on Facebook
    • Share on Twitter
Answer
  • Report
Adv

1 Answer

  • Voted
  • Oldest
  • Recent
  1. Salim
    2019-02-27T07:37:35+03:00Added an answer on February 27, 2019 at 7:37 am

    Kuumwa tumbo wakati wa hedhi

    Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.

    *Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili* . Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

    Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

    Takribani nusu ya wanawake wote waliopo katika umri wa kuweza kupata mototo wanakumbana na maumvu wakati wa hedhi, maumivu ambayo huanza siku chache kabla ya hedhi na kuendelea kwa siku kadhaa. Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kawaida lakini kwa wengine maumivu huwa makali sana hadi kupelekea kushindwa kufanya shuguli zao. Hii ni moja ya sababu watoto wa shule kukosa vpindi kwa siku kadhaa. Ili kupata tiba basi wanawake wengi hukimbilia kunywa dawa za kupunguza maumivu na baadhi ya madactari hutoa ushauri wa kunywa vidonge ili kuzuia hedhi ili kupunguza makali ya maumivu, njia zote hizi mbili zikiwa na madhara na pia kutoweza kutoa suluhisho ala kudumu la tatizo husika.

    Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

    • Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.

    • Kuvunja ungo wakati wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo.

    • Kutoka na damu nyingi wakati wa hedhi. (suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba).

    • Wanawake ambao hawajawahi kuzaa.

    *Maumivu ya Tumbo la Hedhi… Sehemu ya Pili*

    Hii inahusisha magonjwa ambayo husababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi. Miongoni mwa magonjwa hayo ni:

    • Endometriosis. Hii ni hali ambayo seli za ndani ya mfuko wa uzazi huanza kuota nje ya fuko hilo, au hta sehemu nyinginezo.

    • Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaoota katika mfuko wa uzazi.

    • PID au Ugonjwa wa uvimbe katika nyonga

    • Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa.

    • Mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

    Baada ya kujua baadhi ya matatizo ya wanawake yanayoweza kusabibisha hedhi inayoambatana na maumivu ya tumbo,

     *hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?* 

    1. Maumivu mara nyingi si makali.

    2. Muumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti

    3. Maumivu zaidi huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo.

    4. Huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.

    5. Kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.

    6. Kupata choo kilaini au hata kuharisha.

    7. Kufunga choo.

    8. Tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu.

    9. Kuhisi maumivu ya kichwa.

    10. Kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.
    *
    *NAAM KWA MAHITAJI YA DAWA ZA ASILI KWA AJILI YA CHANGO NA MAGONJWA MBALIMBALI WASILIANA NAMI KWA WHAT’S APP AMA KUNIPIGIA SIMU*
    +255 710 271 852

    • 1
    • Reply
    • Share
      Share
      • Share on WhatsApp
      • Share on Facebook
      • Share on Twitter
      • Report
Leave an answer

Leave an answer
Cancel reply

Browse

Adv

Sidebar

Promo

  • Usihangaike tena, Tumekuwekea Kampuni zote za kubet katika app moja! Jaribu Sasa

  • Beti kwa mara ya kwanza, ukishindwa unarudishiwa hela yako

  • Tafuta Ajira kiurahisi. Jaribu Sasa

  • Jifunze jinsi ya kubet kibingwa

  • Explore

    • Home
    • Maswali
    • Polls
    • Points
    • Watumiaji
    • Miongozo
    • App

    MojaSky | Designed by ChuiTec.

    Insert/edit link

    Enter the destination URL

    Or link to existing content

      No search term specified. Showing recent items. Search or use up and down arrow keys to select an item.