Kwa nini Ajibu amekataa kwenda Tp Mazembe?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Musa Adam
Tetesi zinasema hivi kama zilivyoandikwa katika mtandao wa bongo5
Tetesi hizo za kutakiwa kusajiliwa kwa Ibrahim Ajibu zimeshindikana kutokana na klabu ya Simba kutaka kukaa meza moja na TP Mazembe kwaajili ya dili hilo kwakuwa miamba hiyo ya soka ya Msimbazi ilishafanya naye mkataba wa awali na mchezaji huyo.
Inadaiwa kabla ya Mei 23 Meneja wa Ajibu aliwasiliana na klabu ya Simba kuwaaomba wamuruhusu Ajibu ajiunge na TP Mazembe kwa sababu alikuwa amesaini mkataba wa awali na klabu hiyo ndipo klabu ya Simba ikawaambia TP Mazembe waje kwenye meza ya mazungumzo kwa sababu wao wana mkataba wa awali na Ajibu na alishachukua baadhi ya fedha za usajili.
Simba wakawaambia TP Mazembe kuwa Ajibu anauzwa dola 100,000 ambazo ni zaidi ya milioni 220 za Kitanzania na kuwapa sharti la kuweka kwenye mkataba wake iwapo atauzwa klabu nyingine asilimia 20 ya mauzo yake wapate Simba. Ndipo TP Mazembe ikasitisha mpango wa kumsajili kwa sababu wenyewe walikuwa wanajua Ajibu ni mchezaji huru.
Na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera nae alisikika akisema haya
“Kwangu nadhani kakataa kwa sababu moja, labda anaona hapa kila siku anaandikwa kwenye magazeti yote, akipita mitaani watu wanamwita na kumsifia lakini kule mambo hayo hayatakuwepo kunama-star wengi.”
“Au anaogopa akienda kule hatocheza, kama amekataa kwenda ili abaki hapa sawa lakini mimi hawezi kunidanganya, Mazembe wataniambia kilakitu.”