Kuokoka ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Mtu anaokoka kwa kumwamini Yesu Kristo moyoni mwake; ya kuwa ni Mungu aliyefanyika mwanadamu, wala hakutenda dhambi katika uanadamu wake, na ya kuwa aliteswa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, akafa msalabani, akazikwa, na siku ya tatu akafufuka, akapaa juu mbinguni, na sasa yu hai milele ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba.
Mambo haya kumuhusu Yesu na Yesu mwenyewe yanapotoka kuwa ni swala tu la ufahamu alionao mtu akilini au kichwani mwake ikafikia hatua akayapokea moyoni mwake na kuyaamini kisha kuyatii kwamba ndivyo yalivyo, mtu huyu anakuwa amempokea Yesu Kristo ya kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake mara tu baada ya kuomba sala ya toba katika msingi wa imani hii. (Yohana 3:14 – 18; Warumi 10:9 – 10.)
Wokovu ni tendo la rohoni na kwa sababu ni tendo la rohoni linahusisha imani ya mtu juu ya Yesu Kristo ili kuupokea wokovu huo; ni kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo Yesu (Yohana 1:14; Waefeso 2:8, 9) na si kwa matendo yetu wenyewe.
Promo – AjiraSearch
Ajira ya Ndoto Yako
Sasa kutafuta ajira ni rahisi zaidi kwa kutumia app hii.
Tazama AppRickyllobbe
Kuokoka ni imani ya wakristo ambayo maana yake ni kumkiri,kumtumikia na kumfuata YESU KRISTO