Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Neno la Mungu katika andiko la 1PETRO 4:2-5. Linatufundisha na kutuonya waziwazi kuwa mbali kabisa na ulevi na kutumia vileo. Kabla ya kuokoka hapo mwanzoni yamkini tulikuwa tunaishi katika maisha ya ulevi na kutumia vileo na mambo mengi ya tamaa ya uasherati au uzinzi. Hayo ni maisha ya gizani kabla ya kuokoka. Lakini baada ya kuokoka tunakuwa tumetolewa huko gizani na kuingizwa nuruni. Neno la Mungu limetuonya hatuwezi tena kuendelea kuyaishi yale maisha ya gizani ya kuwa wenye tamaa, walevi na kutumia vileo nakadhalika. Tumekatazwa! Na wale wanayoyashiriki hayo ya ulafi, ULEVI na VILEO. Mungu atawahukumu kabisa!
HUWEZI KUSEMA UMEOKOKA huku unaendelea kunywa pombe. Eti kunywa kidogo usilewe! La hasha!
Kuna watu wengi ambao watawafundisha watu na kusema kunywa pombe kidogo usilewe siyo dhambi. Kuzoelea na kunywa pombe kupita kiasi/kiwango ndio dhambi . Lakini ukitimia pombe kwa kiasi siyo dhambi, haina shida.
Na watatumia maandiko yao katika Biblia kwa kuyatafsiri isivyo kiupotofu, ili kuwapotosha waumini wao , kwa kuihalalisha pombe .
Wachungaji, maaskofu, waanijilisti, waalimu au hao wanaojiita watumishi wa Mungu wanaojaribu kuitetea pombe kwa namna yoyote ile iwe kidogo au sana. Hao ni watumishi uchwara tu, ni maajenti wa shetani. NI WAPOTOSHAJI WAKUBWA katika kanisa wanaotumiwa na Ibilisi kuzipoteza roho za watu kwa mafundisho yao potofu kinyume na ukweli wa Neno la Mungu Biblia.
1 TIMOTHEO 4:1-2:-” Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, WAKISIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo , wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe”.
2 PETRO 2:1-3:-“Lakini kuliondokea MANABII WA UONGO katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako WAALIMU WA UONGO, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu KWA MANENO YALIYOTUNGWA; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii”.
Mtu yoyote anayetetea pombe kwa kuhailalisha eti kwa kiasi , huyo ni mtumishi wa Mungu fake anayeingia kwa wewerevu wake UZUSHI WA KUPOTEZA kinyume na ukweli wa maandiko kimsingi.
Lakini ukweli halisi ni kwamba HAKUNA MAHALI POPOTE AMBAPO BIBLIA IMEIHALALISHA POMBE kwa namna yoyote iwe kwa matumizi ya sana au kidogo , kupita kiasi/kiwango au kutovuka kiwango/kiasi. Bado mbele za Mungu hata kuionya tu pombe ni kosa, ni dhambi.
Huo ndio ukweli halisi wala mtu awaye yote asije kukudanganya wewe usomaye ujumbe huu.
Biblia inakuambia katika WAKOLOSAI 2:4,8:-” Nasema neno hili, MTU ASIJE AKAWADANGANYA kwa maneno ya kushawishi. Angalieni MTU asije akawafanya mateka kwa Elimu yake ya bure na MADANGANYO MATUPU, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.”
Narudia tena kwa msisitizo Mkubwa watumishi wanaoilahalisha pombe kwa namna yoyote ile. HAO NI WAPOTOSHAJI NA VIPOFU WA KIROHOwanaotumiwa na Ibilisi kuwadanganya watu au kulipotosha kanisa. Mkristo uliyeokoka uwe makini!
Promo – AjiraSearch
Ajira ya Ndoto Yako
Sasa kutafuta ajira ni rahisi zaidi kwa kutumia app hii.
Tazama AppRickyllobbe
Kunywa pombe sio dhambi lakini dhambi ni matendo utakayoyafanya baada ya kunywa pombe