Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
KUNYWA TU POMBE NA KULEWA POMBE VYOTE NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU.
Kama ni wanafunzi wazuri wa Biblia. Tutafaham kwamba NENO LA MUNGU katika maandiko limetupiga marufuku sio kwamba tusilewe pombe bali hata tusiiguse kabisa pombe vinywani mwetu. Yaani TUSIINYWE KABISA.
Biblia inasema katika maandiko ya fuatayo:-
MITHALI 23:19-20:-” Sikia mwanangu, uwe na hekima, Nakuongoza moyo wako katika njia njema. USIWE MIONGONI MWAO WANYAO MVINYO (pombe); miongoni mwao walao nyama kwa pupa”.
KUMBUKUMBU 29:5-6:” Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani asema BWANA; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako. Hamkula mkate, WALA HAMKUNYWA DIVAI, WALA KILEO (pombe); ili mpate kujua kwamba, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.”
ISAYA 5:11-12, 22, 24:- ” OLE WAO wamkao asubuhi na mapema wapate kufuata kileo: wakishinda sana hata usiku wa manene mpaka Mvinyo imewaka kama moto ndani yao! Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi na mvinyo, zote zi katika karamu zao; lakini hawaingalii Nazi ya BWANA wala kuyafikiri matendo ya mikono yake. OLE WAO walio hodari KUNYWA KILEO CHENYE NGUVU, watu waume wenye nguvu kuchanga vileo (pombe). Ole wao. Kwahiyo kama vile mwali wa moto uteketazao mabua makavu, na manyasi makavu yaangukavyo KATIKA MWALI WA MOTO ; kadhalika shina lao ( hao wanywao pombe) litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake yeye aliye Mtakatifu wa Israeli”.
Mstari huo unaeleza waziwazi kabisa kwamba watu wale wote wanaokunywa pombe (vileo) . Kwa kufanya hivyo wamemdharau Mungu aliye Mtakatifu. Na pia mwisho wao hao walevi wanaokunywa pombe ni kutupwa jehanamu ya moto.
MATHAYO 24:48-51:-” Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula NA KUNYWA PAMOJA NA WALEVI; bwana wake mtumwa Huyo atakuja Siku asiyodhani, na saa asiyoijua, ATAMKATA VIPANDE VIWILI (Huyo mnywa pombe), na kumweka fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
ISAYA 24:9:-” Hawatakunywa divai pamoja na nyimbo; KILEO KITAKUWA UCHUNGU KWAO WAKINYWAO, asema Bwana”.
HESABU 6:1-3:-” Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Nena na watu wa Israel, uwaambie, mtume mume au mtu mke atakapoweka Nadhiri kubwa, nadhiri ya mnadhari, ili ajiweke wakfu kwa BWANA; ATAJITENGA NA DIVAI NA VILEO ; HATAKUNYWA SIKI YA DIVAI, WALA SIKI YA KILEO(Pombe)……”
WAAMUZI 13:4, 13-14:-“Basi sasa, Jihadhari nakuomba, USINYWE DIVAI WALA KILEO (POMBE), wala usile kitu kilicho najisi. Malaika wa Mungu akamwambia Manoa, katika hayo yote niliyomwambia huyo mwanamke na ajihadhari……….WALA ASINYWE DIVAI , WALA MVINYO, wala asile kitu chochote kilicho najisi; hayo niliyomwamuru na ayatunze.”
LUKA 1:13, 15:-” Lakini yule malaika akamwambia usiogope, Zakaria, maana dual yako imesikiwa, na mkeo Elizabeth atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; HATAKUNYWA DIVAI WALA KILEO (POMBE); naye atajwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.”
WAEFESO 5:18:-” Tena MSILEWE KWA MVINYO, ambamo mna ufisadi; Bali mjazwe Roho”.
Unaweza kuona mpaka hapo. Neno la Mungu Biblia imetuonya kabisa na kutupiga marufuku sio kulewa tu kwa kutumia pombe kupita kiasi ndio dhambi. Hapana. Bali hata kunywa tu mdomoni ni dhambi vilevlile iwe kwa mantiki ya kulewa au pasipo kulewa kabisa. Bado ni dhambi na machukizo mbele za Mungu. Utakwenda jehanamu ya moto.