Kuna faida gani katika kujitolea?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Salim Jumbe
Kujitolea ni kutoa sehemu ya muda wako, ujuzi na maarifa uliyonayo na wakati mwingine nguvu zako kufanya kazi ya watu wengine bila kupata malipo ya moja kwa moja. Tuangalie kwa mhutasari kwa nini ni muhimu kujenga tabia ya kujitolea.
Kusaidia kutatua matatizo ya jamii
Kujitolea, kwa mantiki hii, ni kuelewa kuwa si lazima ubadilishane ujuzi na muda wako kwa vipande vya fedha. Wakati mwingine waweza kutoa ujuzi, maarifa na nguvu zako kwa lengo tu la kujisikia furaha ya kutoa mchango wako katika kuboresha maisha ya wengine ambao katika hali ya kawaida wasingeweza kunufaika na ujuzi huo bila kukulipa.
Kujifunza ujuzi bila gharama
Katika mazingira haya, kujitolea hutusaidia kujifunza ujuzi mahususi tunaouhitaji ili kuajirika kirahisi bila kulazimika kuulipia kwa fedha isipokuwa kwa kutumia nguvu na muda wetu. Kwa mfano, mhitimu wa teknolojia ya mawasiliano anaweza kujitolea kufanya kazi katika kampuni ya mawasiliano na hivyo kujifunza mambo mengi ambayo huenda hakujifunza akiwa chuoni. Kwa kutoa muda na nguvu zake bila kutarajia malipo, mhitimu huyu hupata faida ya kujiongezea nafasi ya kuajirika pale nafasi za kazi zinapojitokeza.
Kujitafutia uzoefu unaohitajika
Ni vyema kutambua kuwa waajiri huvutiwa na mwombaji kazi aliyetayari kujitolea. Mwombaji mwenye historia ya kujitolea muda na ujuzi wake kuwanufaisha wengine anakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushindana na wenzake wasiojitolea. Kujitolea kwaweza kuwa namna ya kuongeza uwezekano wa kuajirika.
Kujiongezea mtandao wa kiajira
Kujitolea kwaweza kumsaidia mtafuta ajira wa aina hii kujiongeza kimtandao. Unapokuwa tayari kufanya kazi za kujitolea kwa bidii na maarifa katika maeneo mbalimbali, mathalani, unakutana na watu wa kada na wenye uzoefu tofauti. Ingawa ni kweli hupati kipato unachokihitaji (sana) kwa wakati huo, lakini bado unakuwa na fursa ya kujitengenezea mtandao muhimu wa watu wanaoweza kukufaa katika safari yako ya kutafuta ajira.
Soma kwa urefu zaidi hapa