Kuna aina ngapi za Biblia?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Biblia ni moja tu, sema kutokana na tafsiri tofauti tofauti na baadhi ya kugawanyika kwa makundi ya wakristo kumetokea aina kadhaa za Biblia japo zote zinaeleza hadithi na mafunzo ya Mungu. Kuna hizi
Biblia ya Kiprotestanti (Protestant Bible)
Hii ndio Biblia inayofahamika zaidi. Ina vitabu 17 vya historia katika agano la kale, vitabu vitano vilivyokaa kiushairi na 17 vya manabii. Agano jipya lina vitabu 4 vya injili, vitabu 21 vya waraka na kitabu cha ufunuo. Kwa hiyo jumla kuna vitabu 66.
Biblia ya Katoliki (Catholic Bible)
Biblia ya Katoliki ina jumla ya vitabu 73, ina vitabu 7 ambavyo havipo katika iyo iliyotajwa hapo juu na ina nyongeza ya maandiko katika vitabu vya Esta na Danieli Vitabu vilivyoongezeka ni Tobiti, Yudith, Wamakabayo I, Wamakabayo II, Hekima na Yoshua bin Sira
Biblia ya Wayahudi (Jewish Bible)
Hii Biblia inajulikana kama Torati. Ni muunganiko wa vitabu vitano vya Musa, 8 vya unabii na 11 vya maandiko ambavyo ni Zaburi, Mithali na Wimbo ulio bora.
Biblia ya Anglikana (Anglican Bible)
Hii Biblia ina vitabu vyote vya Agano Jipya pamoja na vitabu vya Wayahudi vya Agano la kale la zamani. Haijaweka vitabu 15 ambavyo vinapatikanakatika Biblia ya Kiproestanti.
Biblia ya Orthodox ya Ugiriki (Greek Orthodox Bible)
Hii ndo Biblia kubwa zaidi. Ina mkusanyiko wa vitabu vyote ikiwemo vya Biblia ya Katoliki, vitabu vya Wakristo wa Orthodox kama Wamakabayo wa 3, Wamakabayo wa 4 na Zaburi 151.
Chanzo