Kitu gani kimekukasirisha leo?
Pinned
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Faustine John
Kuna binti flani nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa muda kama wa wiki mbili sasa. Nakumbuka kipindi namtongoza alinipa sharti ya kwamba asijue mtu yeyote hata Rafiki yangu wa karibu ambaye pia ana mazoea naye.
Kwakuwa ndo ilikuwa ni mwanzo nikasema nikaushe tutajua mbele kwa mbele, ingawa nilikuwa na mashaka na tabia zake.
Mahusiano yetu yalivoendelea kuna baadhi ya watu walianza kujua taratibu na wengi walihisi. Sasa leo ikiwa ni wiki ya pili nimeamka zangu kama kawaida saa 2 nikamtumia text.. Kimyaaa, saa 4 tena.. Kimyaaa, saa saba nimempigia hajapokea nikaamua niingie Whatsapp.. huko naona Last seen saa 10.
Sasa mida ya saa 12 napokea namba mpya.. kidogo anapokea yeye anasema eti ooh naumwa ndo mana sijakucheki siku nzima. Hapa nimemmind kichizi na sijamjibu wala nini na ninahisi sitakaa niongee naye tena .
kutoka facebook