Mtandao maarufu wa WhatsApp ulitambulisha kwa watumiaji wake njia mpya ya kushea picha, video au mawazo mbalimbali. Njia hiyo inayujulikana kama WhatsApp Status

Ili kufaidi zaidi njia hii ni vema ukajua vitu kama namna unavyoweza kurudisha nyuma/kuangalia picha au video iliyopita bila kufuata tena mtiririko wa mwanzo.

Unaweza kurudisha nyuma au kupeleka mbele status unayoingalia.

Unachotakiwa kufanya ni kugusa/kubonyeza eneo la usawa wa katikati kushoto kurudisha nyuma na kulia kupeleka mbele.

  

Upande wa mkono wako wa kushoto unarudisha nyuma na unaweza kupeleka mbele kwa usawa wa mshale wa kulia au sehemu nyingine yoyote ya screenyako.

Njia hii inatumika kwa picha, video au status ya maneno.