Huenda umekuwa ukijiuliza kama kuna faida yoyote ya kuwa na kurasa(page) ya facebook. Napenda kukujuza kuwa kuna faida kubwa ya kuwa na ukurasa wa facebook. Moja ya faida ikiwa ni eneo la kukutana na wateja wa bidhaa au huduma yako.

Hatua za kufata kufungua page yako
KOMPYUTA
  • Ingia katika kivinjari(browser) yako kisha ingia katika tovuti ya facebook kisha fungua acccount(sign up) au ingia katika account yako(log in)
  • Tafuta eneo liloandikwa ‘create’ kisha bonyeza neno ‘page’ lililo chini yake

 

                                               
  • Hatua inayofata ni kuchagua aina ya page unayotaka kufungua. Kwa mfano mimi nimechagua “brand or product” kisha aina ndogo yani sub category ya “website”

  • Baada ya hapo andika jina la page unayotaka kufungua mfano “Mojasky WEB” kama inavyoonekana katika picha chini kisha bonyeza “Get Started”

  • Mpaka hapo unakua umemaliza kufungua page yako. Unaweza kuendelea na hatua zinazofata au ukaachana nazo kwa kubonyeza neno ‘SKIP’

 

SIMU(KWA KUTUMIA FACEBOOK APP)
  • Ingia katika app yako ya facebook (hakikisha umejiunga au umeigia katika akaunti yako ya facebook) kisha bonyeza alama ya mistari mitatu iliyopo juu pembeni ya sehemu ya ‘notifications’ kisha tafuta neno create a page na ubonyeze neno hilo

  • Baaada ya kubonyeza neno hilo itatookea page kama inaayoonekana hapo chini. Bonyeza ‘Get Started’
  • Andika jina kwa ajili ya page yako mfano ‘Mojasky tz’
  • Kisha chagua aina na aina ndogo ya page zako (angalia mfano katika picha chini) kisha bonyeza neno ‘NEXT’ kumaliza hatua za kufungua page yako. 
  • Unaweza kuendelea na machaguo yanayofata au unaweza kuacha na ukafanya badae kwa kubonyeza neno ‘SKIP’ (Machaguo yanayofata ni kama ku-upload profile pica au picha ya kava)