Ili ufurahie zaidi matumizi ya simu yako ya Android ni vyema kuongeza idadi ya applications au games. Kuna njia nyingi za kudownload apps hizo katika simu yako ya Android.

Njia 3 za kudownload
1.Google Playstore

Ingia katika app yako ya Google playstore kisha tafuta(search) app uipendayo kisha bonyeza kitufe cha ku-download.
Faida ya ku download apps kwa njia hii ni uhakika wa usalama wako na kifaa chako(simu yako).

2.App store nyingine

Unaweza pia kudownload apps/games kupitia store nyingine kama Amazon store na Mobogenie Store.
Kabla ya ku-install apps kutoka store nyngine kumbuka kuruhusu (apps from unknown sources) nenda
settings>>security>>unknown sources 
kisha washa.

3.Apk katika internet

Njia nyingine ni ya kwenda katika kivinjari(browser) yako na ku-search jina la app yako na mwisho malizia na neno apk mfano facebook apk kisha chagua link moja na ifate kwa ajili ya kudownload.

Kumbuka

Kwa kutumia njia namba 2 na namba 3 hapo juu unaweza kudownload apps fake au zisizo salama kwa simu yako. Inapendekezwa/ni vyema kutumia njia namba 1.