Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Neno la Mungu linatufundisha umuhimu wa kufanya mazoezi ki-mwili. Tena wataalamu wanasema mazoezi ni Afya. Biblia inasema katika
1 T I M O T H E O 4:8:-
“Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye”.
Mstari huo katika tafsiri ya kiingereza ya New Kings James Version, unasomeka hivi :-
1 T I M O T H Y 4:8:-
” For BODILY EXERCISE profit a little, but godliness is profitable for all things, having promise of the life that now is and of that which is to come”
Kwahiyo kufanya mazoezi ya aina yoyote ya viungo kwa lengo la kuimarisha Afya ya mwili wako. Ni kitu chema na kilicho katika mapenzi ya Mungu. Biblia inaendelea kusema :-
3 Y O H A N A 1:2
” Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote NA KUWA NA AFYA YAKO , kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
NB
Ni muhimu kuweza kuelewa vizuri na kutofautisha. Unapoamua kufanya mazoezi ya kucheza mpira wewe kama wewe kwa lengo tu la kuuweka mwili wako sawa ki-afya, kufanya hivyo siyo dhambi .
Lakini mpira unapochukua sura nyingine ya ligi za mashindano ya mechi. Hapo ndani yake kunakuwa na matatizo makubwa ambayo huzaa dhambi nyingi zitokanazo na mpira. Biblia inasema katika WAFILIPI 2:3:-” MSITENDE NENO LO LOTE KWA KUSHINDANA wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu , kila mtu na amuhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake”. Hatupaswi kufanya NENO LOLOTE KWA KUSHINDANA ili nani aonekane yeye ni bora zaidi kuliko mwingine. Mungu hayuko katika hali hiyo. Na Kama watu tuliookoka kwa msingi huo pia hatupaswi kushiriki wala kujihusisha na mashindano ya ligi/mechi za mipira.
Tucheze mpira kama mazoezi tu lakini tusicheze mpira kama mashindano fulani. Tusishabikie mpira wala kujihusisha na mashindano ya ligi za mpira. Kupitia mashindano ya ligi za mechi huzaliwa dhambi nyingi kama vile Rafu, ugomvi, bifu, matusi, fujo, kiburi, tamaa, ubaya n. k. Hapo tena sio mazoezi bali ni kitu kingine kinachotafutwa.