#Kwanza tukubali sio kila mwenye kompyuta ya apple anatumia simu ya iPhone. 

Zifuatazo ni njia rahisi za kuhamisha vitu vyako kutoka kwenye Android kwenda kwenye kompyuta ya apple.
  • Washa mtandao kwenye kompyuta yako ya apple ili uweze kuingia internet kwa ajili ya kudownload application inayoitwa “ANDROID FILE TRANSFER” 
  • Application hii inapatikana mahali tofauti tofauti lakini kupitia link inayoonekana hapo chini kwenye picha itakua rahisi zaidi.

     

  • Andika link hiyo na itakupeleka moja kwa moja kuidownload . Tazama picha hapo chini.
  • Ikimaliza utaenda kwenye kompyuta yako sehemu ya download na utakuta android file transfer.
  • Kisha fungua “click and drag” kwenda kwenye application folder. Hapo utakua umemaliza hadi kufanya installation.
  • Utabonyeza palipoandikwa open kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Sasa unaweza kuchomeka simu yako ya Android kwenye kompyuta yako ya apple na kuendelea kuhamisha vitu kutoka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta na kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye simu.
HAKIKISHA SIMU YAKO HAIJAWEKWA LOCK WAKATI UNAUNGANISHA KWENYE KOMPYUTA YAKO.