Haiba ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. Haya yote hujenga mwonekano wa mtu unaopimika (tabia) kama vile anavyoongea na watu, anavyodhibiti hasira zake, anavyofanya maamuzi, anavyoweza kuwa mwaminifu, anavyoweza kutunza siri moyoni, anavyoweza kukabiliana na changamoto, anavyovaa na mambo kama hayo mengi mengi mengi.
Haiba hii tunayoizungumzia hujengwa na mambo mengi. Tunaweza kutaja kurithi kama sehemu muhimu ya utengenezaji wa haiba. Hapa tunazungumzia kemikali zinazoongoza mienendo ya mwili ama homoni (kwa kutohoa). Ujue wingi ama uchache wa homoni fulani huchangia kujengeka kwa tabia fulani. Pia mazingira alimokulia mtu, kwa maana ya watu na malezi aliyopata na kadhalika.
Vile vile ni vyema kujua kuwa haiba ya mtu hubadilika kuendana na umri. Kila umri unazo changamoto zake zinazoathiri haiba ya mtu husika. Haiba yangu nilipokuwa na umri wa miaka mitano siyo niliyokuwa nayo nikiwa na umri wa miaka kumi na mitano na siyo niliyo nayo hivi sasa. Kwa sababu haiba yangu inabadilika kwa umri. Nikioa haiba yangu pia itabadilika…. endelea kusoma hapa Bwaya blog