Game la mpira bora zaidi ni lipi?, linapatikana wapi?, kwa nini ni bora zaidi?. Endelea kusoma na utapata majibu ya maswali yote hayo kadri unavyoendelea.

Game la mpira bora zaidi ni lipi?

Dream League Soccer(DLS). Kati ya magemu yote ya mpira niliyowahi kucheza katika simu yangu  Dream League Soccer ndio game bora zaidi kwa vigezo nilivyokua nimeviweka.

Kwa nini DLS ndio game bora zaidi?

Kuna sababu nyingi zinazosababisha nitoe nafasi hii kwa DLS licha ya uwepo wa magemu mengine

  1. Unapata experience ya soka halisi kutokana na uwepo wa wachezaji halisi kabisa. Japo hii inapatikana pia katika games nyingine ila ni moja ya sababu.
  2. Linahitaji space ndogo(lina mb chache). Hauhitaji nafasi kubwa katika simu yako au kutumia kiasi kikubwa cha kifurushi chako kudownload game hili kutokana na udogo wake. Ni kama mb 300 ukilinganisha na mengine yaliyo na kama gb 1 na kuendelea
  3. Ni rahisi zaidi katika kucheza. Siongelei urahisi wa mechi bali nazungumzia kuelewa vitu unavyohitajika kufanya kama kununua au kuuza wachezaji na mengine mengi.
  4. Kuna mtiririko mzima wa mechi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hapa unaona matukio yote ya mechi ikianza hadi mwisho ukilinganisha na games nyingine ambazo matukio yapo kwa vipande vipande.
Game hili linapatikana wapi?

Sehemu bora zaidi ya kulipata game ili ni kwenye Google PlayStore. Lakini unaweza kulipata kwa kusearch tu internet au sehemu kama uptodown softonic au mobogenie store

Kwa nini Google PlayStore?

Kwa sababu unakuwa na uhakika wa kudownload game halisi likiwa full na usalama wa kifaa chako pia ni uhakika. Kwa kutumia njia nyingine unaweza kudownload game nusu na usijue jinsi ya ku install baadae.

Nifanyeje ili kupata coins nyingi zaidi?

Njia ya kwanza ni kununua coins hizo kwa pesa halali ndani ya game hilo. Lakini pia kuna njia rahisi ya kufanya hivyo bila kutumia pesa lakini sio halali kuitumia angalia hapa

Game hili lina udhaifu gani?

KIla kizuri hakikosi udhaifu. Graphics katika game hili ni za kuridhisha lakini zinazidiw sana na game kama PES. NA pia katika swla la uhalisia wa wachezaji apo FIFA ipo juu zaii ya DLS. KAtika gemu hili pia ni ngumu sana kutafuta hela kwa njia ya kawaida ya game.

Sipendi DLS game gani zuri zaidi?

Kama hutopenda chaguo hili napendekeza uchukue FIFA Football au PES Mobile