Faida za mafuta ya mawese kwenye ngozi ni zipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Please briefly explain why you feel this question should be reported.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Please briefly explain why you feel this user should be reported.
Mafuta ya mawese ama palm oil yana faida nyingi tu kwa ajili ya ngozi yako
Yanalainisha ngozi na kuiacha ikiwa na unyevu unyevu
Siku hizi sabuni, shampoo na mafuta mengi yanayotengenezwa viwandani yanakua yanatumia mafuta ya mawese kama malighafi ya kutengenezea. Hii ni kwa sababu ya ubora wake na suluhisho katika maswala yanayohusu ngozi.
Yana virutubisho vinavyoweza kuponesha ngozi iliyochomwa na jua na yenye michirizi.
Kama ilivyo kwa mafuta mengine halisi mafuta ya mawese ni bora sana kwa kuwa na virutubisho ambavyo ni asilia yani natural
Vitamin E
Haya mafuta yana vitamin E inayojulikana kama tocotrienols. Tocotrienols imefanyiwa utafiti na ikagundulika kuwa ina nafasi katika kuishinda saratani(cancer) na magonjwa ya ubongo na moyo.
Pia inasaidia kujikinga na jua kali na kupunguza makovu. Hii ni kutokana na faida za tocotrienols iliyotajwa hapo juu.
Vitamin K: Hii inasaidia ngozi iweze kuwa na uwezo zaidi wa kujiponya yenyewe mfano katika vidonda vidogo dogo na kupona haraka baada ya kufanyiwa upasuaji.
Glycolipids: Hii inasaidia kuifanya ngozi kuwa vizuri kuepuka ngozi kukakamaa au kuwa na ngozi ya uzee.