Mara nyingine unaweza kuvutiwa na status ya whatsapp iliyowekwa na ndugu au rafiki na huenda ukaihitaji bila kumjulisha au kumuomba akutumie. Kwanza kabisa ni lazima uwe ume install Whatsapp katika simu yako. Kama bado soma Njia 3 za ku-install WhatsApp kwenye simu ya android

Hii ndio njia rahisi ya kuipata status hiyo bila kutokwa na jasho.

  • Ingia katika application yako ya file manager/file explorer kisha ingia katika folder la ‘whatsapp’. Linaweza kuwa katika Phone Storage au SD Card.
whatsapp folder
  • Kisha chagua “Media”.
whatsapp media
  • Baada ya hapo bonyeza alama ya nukta tatu kama inavyoonekana katika picha hapo chini.

 

  • Bonyeza “Show hidden files”. Hapa unaonesha picha na video ambazo app inasevu ila zinakua hazionekani.
show hidden files
  • Utaona mafaili yameongezeka ikiwemo faili la ‘Statuses’. Katika faili hii ndipo status zako huwa zinahifadhiwa. Bonyeza kufungua.
statuses
  • Baada ya kubonyeza faili la ‘Statuses’ utaona picha video au vyote. Unaweza kuangalia au kuhifadhi kwa kukopi na kupesti au kuhamisha kabisa katika folder hilo kwenda lingine

 

KUMBUKA

Kama ukiacha video au picha katika folder hilo hilo status hizo huwa zinafutika baada ya muda fulani.