Divai/mvinyo ni nini?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
UFAFANUZI KUHUSU NENO MVINYO, DIVAI NA KILEO KATIKA BIBLIA.
Neno Divai, Mvinyo au kileo ( WINE) limetajwa katika Biblia nzima zaidi ya mara 234.
Katika Biblia yetu ya kiswahili hatuwezi kukuta neno hili “Pombe“. Lakini badala yake maneno yanayotumika kuizungumzia pombe katika Biblia yanasimama kama Mvinyo, Divai au kileo kwa eneo la upande mmoja.
NB:-
Ijapokuwa kwa upande wa pili vile vile. SIO KILA NENO MVINYO au DIVAI linapotumika katika mistari ya Biblia linamainisha pombe kama pombe. Hapana.
Kuna mahali pengine katika maandiko ya Biblia limetafsiriwa neno MVINYO/DIVAI lakini haina maana ya pombe kama pombe kwa namna ile inavyofahamika kwa wengi . Lakini ukirudi katika LUGHA YA ASILI YA BIBLIA ya kiebrania na kiyunani, neno lilotumika hapo halimainisha pombe kama pombe hasa ( Alcoholic drink). Ingawa kwa kiswahili wametafsiri mvinjo au Divai.
Kuna maneno zaidi ya 11 tofauti ya kiebrania yanayotumika kuelezea kinywaji kinachotokana na zabibu. Sasa ingawa katika Biblia ya kiswahili au kingereza limetumika neno moja tu MVINYO au WINE.
Nimesema sio kila neno mvinjo au Divai linapotumika katika Biblia linamainisha pombe moja kwa moja . La hasha!
NENO MVINYO/ DIVAI au WINE linapotafsiriwa katika Biblia. Limetokana na neno la kiebrania “YAYIN” na kiyunani “OINOS“. Ambapo haya ni maneno ya jumla yanayotumika kuilezea ile divai iliyochachuka tayari ( Pombe) na ile Divai ambayo bado kabisa haijachachuka (fesh grabe juice).
Kwa hiyo SIO KILA NENO mvinyo/Divai linapotumika katika mistari ya Biblia inamainisha pombe. Mahali pengine inaweza ikamainisha mvinjo pombe na mahali pengine mvinyo isiwe na maana ya pombe.
KWA MFANO.
Katika MWANZO 27:28, 37, Biblia inasema :- ” Mungu na akupe umande wa mbinguni, Na ya manono ya nchi, na wingi wanafaka na MVINYO. Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake ; kwa nafaka na MVINYO nimemtegemeza……”
Sasa kwa haraka haraka unaweza kufikiri mvinyo uliotamkwa hapo ni Pombe. Jambo ambalo siyo kweli.
Neno mvinyo lilotafsiriwa hapo limetokana na neno la kiebrania ambalo ni ” TYROSH”. Na neno hilo maana yake ni “FRESH GRAPE JUICE”. Ni juice fresh tu ya zabibu iliyotumika hapo na siyo pombe.
Sijui unaweza kunielewa mpaka hapo!!
Mfano mwingine.
MITHALI 3:10:-” Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi; na mashinikizo yako yatafurika DIVAI MPYA”.
MIKA 6::15:-” Utapanda lakini hutavuna; utazikanyaga zeituni, lakini hutajipaka Mafuta; na hizo zabibu, lakini HUTAKUNYWA DIVAI“.
ISAYA 65:8:-” BWANA asema hivi, kama vile DIVAI MPYA ipatikanayo katika kichala, na mtu mmoja husema, usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake; ndivyo nitakavyotenda kwa ajili ya watumishi wangu, ili nisiwaharibu wote”.
Neno DIVAI iliyotajwa hapo kiebrania ni “TYROSH”. Ambalo maana yake ni kinywaji cha juice fresh ya zabibu.
Ambapo Mungu mwenyewe amesema hapo kinywaji cha namna hiyo, kinakuwa kina baraka ndani yake. Mungu anakikubali tukitumie .
Hata katika ushirika wa meza ya BWANA, ni makosa kutumia pombe (wine). Bali inapaswa itumike tu juice fresh ya zabibu ambayo haina Alcoholic. Na ndiyo Divai ya namna hii iliyotumika katika MATHAYO 26:26-29.
MFANO MWINGINE
Biblia inasema MWANZO 9:20-24:-” Nuhu akaanza kuwa mkulima , akapanda mizabibu: AKANYWA DIVAI , akalewa , akawa uchi katika hema yake. Hamu baba wa kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje”.
MITHALI 23:30-32:” Ni wale wakaao sana kwenye MVINYO: waendao kutafuta DIVAI Iliyochanganyika. USIITAZAME MVINYO iwapo ni nyekundu; Itiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; mwisho wake huuma kama nyoka: huchoma kama fira”
Sasa neno DIVAI au MVIYO uliotumika katika mistari hiyo . Linatokana na neno la kiebrania ” YAYIN” iliyokwisha kuchachuka na kufikia hatua ya kuwa nyekundu. Ambapo kiufupi imekuwa ni Pombe tayari. Sasa
Na ikishakuwa Pombe , Biblia imepiga marufuku hapo ikisema USIITAZAME . Maana yake usijaribu kuigusa wala kuinywa huo mvinyo/Divai.
Unaweza kuona mpaka hapo.
Nilichotaka uelewe hapo mpendwa msomaji wangu ni kwamba neno hili DIVAI/ MVINYO (WINE) linapotumika katika Biblia, siyo kila eneo katika maandiko linapotumika linamainisha kuwa ni Pombe moja kwa moja . La hasha!!
Kwa ufupi Divai ambayo ni Pombe inaitwa pia ni DIVAI YA JEURI ambayo inatajwa wanaoitumia sio watu wa Mungu bali ni waovu ( MITHALI 4:14-17).
Lakini watakatifu wa Mungu tuliokolewa tunainywa tu ile DIVAI ILIYO NJEMA ambayo inakuwa tu ni juice fresh na siyo pombe. Unaweza kuona mpaka hapo
( YOHANA 2:10-11; ISAYA 65:8 ).
Asante kwa somo nimejifunza kitu kikubwa kuhusu divai/mvinyo
Ubarikiwe mtumishi wa MUNGU
Wanasema hizi dawa za mahospitalini na zenyewe zinahusishwa na divai,ni kweli?