Dalili za ugonjwa wa corona ni zipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Lost your password? Please enter your email address. You will receive a link and will create a new password via email.
Please briefly explain why you feel this answer should be reported.
Fred Moshi
Dalili za ugonjwa wa Corona ama COVID19 ni homa, uchovu na kikohozi kikavu.
Wagonjwa wengine hupata dalili kama misuli kuuma, pua kubana, mafua kutiririka, maumivu ya koo au kuharisha. Dalili hizi huwa ni ndogo na huanza taratibu.
Baadhi ya watu huambukizwa na hawapati dalili yoyote. Katika wagonjwa 100 wa ugonjwa wa Corona wagonjwa 80 hupona ugonjwa wenyewe bila kuhitaji matibabu mkubwa. Ni mgonjwa mmoja kati ya 6 aliyeambukizwa virusi wa Corona COVID19 hupata ugonjwa mkubwa na kupata shida ya kupumua.
Wazee, watu wenye shida nyingine za afya kama shinikizo kubwa la damu, matatizo ya moyo au kisukari huwa na uwezekano wa kupata dalili mbaya. Ni asilimia 2 tu ya watu walioambukzwa virusi vya Corona COVID19 wamefariki. Watu walio na dalili kama homa, kikohozi na shida ya kupumua watafute msaada wa kitiba.
chanzo – medium