Chuo cha Mipango Dodoma – Institute of Rural Development Planning (IRDP) ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 1980 kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 1980.

Chuo kinapatikana Dodoma Mjini pamoja na vyuo vingine kama Chuo kikuu cha Dodoma(University of Dodoma), Chuo cha utumishi wa umma na chuo cha madini dodoma.

Chuo hiki kinatoa kozi 27 na kina wanafunzi wapatao 6000 na wakufunzi 50.

Mawasiliano ya irdp Dodoma

Mkurugenzi ( Dodoma Campus )
S.L.P 138, DODOMA, TANZANIA.

Simu: +255(0) 26230214

E-mail: rector@irdp.ac.tz

Mkurugenzi kanda ya ziwa ( Mwanza Campus )
S.L.P 11957, MWANZA, TANZANIA.

Simu: +255(0) 28 2560994/5

E-mail: mwanza@irdp.ac.tz

au zaidi https://www.irdp.ac.tz/contactus.php

Institute of rural development planning Dodoma application form

Kuapply katika chuo cha mipango Dodoma ingia katika website http://oas.irdp.ac.tz/site/login.aspx

kisha fuata hatua za kujisajili, kulipia na kuchagua kozi.

Chuo cha mipango dodoma joining instructions

Sifahamu kama kuna njia ya moja kwa moja ya kupata joining instructions au admission letter ila nashauri mhitaji kutumia account aliyotumia wakati wa ku apply kwa ku log in hapa au kuulizia information katika page hii

Je ukisoma institute of rural development planning(irdp) utapata mkopo wa bodi ya mikopo Tanzania?

Ndio, mtu yoyote anaweza akapata mkopo ikiwa tu anakidhi vigezo vilivyoainishwa na bodi ya mikopo ya Tanzania katika utolewaji wa mikopo hiyo. Kuwa mwanafunzi wa chuo fulani hakukuongezei nafasi ya kupata mkopo.

Chuo cha mipango dodoma kinatoa nafasi za kazi?

Kama ilivyo kwa taasisi nyingine za serikali na binafsi taasisi hii huwa inatoa nafasi za kazi. Kujua nafasi zikitangazwa tembelea tovuti (https://www.irdp.ac.tz) yao mara kwa mara na sehemu nyingine zinazotoa matangazo ya kazi kama magazeti na tovuti nyingine.