Aina za maombi ya kufunga ni zipi?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Emmanuel Magessa
1. Mfungo kamili
Katika mfungo huu hakuna kula kabisa chakula kigumu bali waweza kunywa maji au kimiminika chochote cha kukusupport.
Siku ngapi waweza kufunga mfungo wa aina hii unategemea na neema na malengo yako katika mfungo huo. Wengine huenda siku moja, mbili, tatu, wiki, n.k n.k
2. Mfungo nusu
Mfungo nusu huanzia saa 12 asbh hadi saa 9 mchana au kuanzia jua linapoibuka hadi linapozama. Mfungo ambao madhehebu mengine wamewazoeza waumini wao kuufanya. Wengine wameweza kuufanya kila ijumaa. Madhehebu ambayo yamewazoesha watu wao kufunga angalau kila wiki mara moja wameweza kuwa na mafanikio makubwa sana katika kuzifungua nira na vifungo mbali mbali
3. Mfungo wa Daniel
Daniel alifunga mifungo miwili ya aina yake;• Katika Sura ya I Daniel alifunga alikula mboga mboga tu (Yaweza kuwa alikula mboga mboga na juisi Fulani Fulani)
• Katika sura ya 10 Daniel alifunga kwa siku 21 kwa kutokula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwake”