Aina gani za wanaume wa kuepuka katika mahusiano?
Jiunge MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Login MojaSky ili uweze kuuliza maswali, kujibu maswali ya watu wengine na kutengeneza connection
Umesahau password yako?. Andika email yako hapo chini alafu bonyeza 'Reset'. Utapokea link katika email yako kwa ajili ya kutengeneza password mpya.
Tafadhali elezea kwa nini unahisi chapisho hili linapaswa kuripotiwa
Jose Mandingo
Hawa ndio aina za wanaume unapaswa kukaa nao mbali.
1. Mwanaume Kicheche:
Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi, lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche.
2. Mwanaume asiye na kazi na asiyejishughulisha:
Mwaume asiye na kazi na asiyejishughulisha ni mzigo usio na mwenyewe. Mwanaume asiyejishughulisha eti kwa sababu hajapata kazi huyo hana malengo. Kukubali kuwa na uhusiano na mwnaaume wa aina hiyo ni sawa na kuishi na mtu mfu anayetembea (dead alive), labda tu kama atakupa sababu inayoingia akilini kuhusu kutokuwa kwake na kazi na kutojishughulisha kwake.
3. Mwanaume asiyejiamini:
Kukubali kuwa na mahusiano na mwanaume asiyejiamini ni sawa na kuishi na bomu ndani ya nyumba. Mwanaume asiyejihisi kuwa yuko salama na mwenye mashaka muda mwingi kuhusu uhusiano wenu, hutawaliwa na wivu wa ajabu ambao licha ya kukuletea fedheha kwa ndugu, jamaa na marafiki zako, lakini pia anaweza kukudhuru au hata kukutoa roho siku moja.
4.Mtoto wa mama:
Inawezekana mwanaume akalazimika kuishi nyumbani kwao kwa muda baada ya kumaliza masomo au amepoteza ajira na akawa bado hajapata ajira au hajapata shughuli ya maana itakayomwezesha kujitegemea, hii inakubalika. Hata hivyo kama mwanamke anakutana na mwanaume ambaye anaishi na wazazi wake na haonyeshi dalili za kutafuta kazi au shughuli yenye kipato itakayomwezesha kuondoka hapo kwao na kujitegemea, usije ukajiingiza katika uhusiano na mwanaume wa aina hiyo.
5. Mwanaume anayependa kutukuzwa kama mfalme:
Unaweza kukutana na mwanaume aliyejipachika kibandiko ufalme ambaye anapenda sana kuhudumiwa kama mfalme. Yaani anataka afanyiwe kila kitu.
6. Mwanaume mwenye utititri wa watoto kila kona:
Mwanaume kuwa na watoto nje ya ndoa si jambo la kushangaza siku hizi, lakini pale unapokutana na mvulana mwenye umri wa miaka 25 lakini ana watoto watatu kwa mama tofauti, mh! hapo sikushauri ujiingize kwenye uhusiano na mwanaume huyo.
7. Mwanaume anayejipenda mwenyewe:
Mwanaume anayejipenda mwenyewe ni kizungumkuti kingine ambacho wanawake wanapaswa kujiepusha nacho.
8.Mwanaume bahili:
Unakutana na mwanaume mtoko wa kwanza tu anakuchagulia aina ya chakula au kinywaji kwa kuangalia bei rahisi na wakati wa kulipa anahesabia hela yake mfukoni, huyo ni janga.
9.Mwanaume chapombe mlevi kupindukia:
Hakuna ubaya mtu kunywa pombe, hasa kama unajua kiwango chako cha unywaji, lakini kuwa na uhusiano na mwanaume mlevi anayekunywa pombe kupindukia kila siku non stop 24/7 huyo hafai.
10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :
Mwanaume mwenye kisirani ni ngumu sana kuishi naye. Mwanaume mwenye kisirani na anayependa kuweka vitu rohoni na asiyeweza kusamehe ni janga.
Kama unataka kusoma kwa urefu zaidi Bonyeza hapa